Kingaanyatjarra

Kingaanyatjarra ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wangaanyatjarra katika majimbo ya Australia Magharibi na Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kingaanyatjarra elfu moja. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingaanyatjarra kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne