Kingala (Kongo)

Kilingala (au Lingala) ni lugha ya Kibantu hasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako ni lugha ya taifa na Jamhuri ya Kongo ambako pia imetambulika rasmi. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kilingala kiko katika kundi la C40.

Kinazungumzwa hasa na Wangala.

Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kilingala kama lugha ya kwanza katika Jamhuri ya Kidemokrasia imehesabiwa kuwa zaidi ya watu milioni 5.5; pamoja na hayo kuna watu milioni saba ambao huongea Kilingala kama lugha ya pili. Tena kuna wasemaji wa Kingala nchini Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gabon, Guinea ya Ikweta, Kamerun, Chad na Angola.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne