Kingayawung kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wangayawung katika jimbo la Australia Kusini. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kingayawung, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingayawung kiko katika kundi la Lower Murray.