Kinimboran ni lugha ya Kipapua nchini Indonesia inayozungumzwa na Wanimboran. Mwaka wa 1987 idadi ya Wanimboran imehesabiwa kuwa watu 3500 lakini walioweza kuzungumza lugha ya Kinimboran walikuwa 2000 tu, yaani walianza kubadilisha lugha, na inawezekana lugha itatoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kinimboran iko katika kundi lake lenyewe la Kinimboran.