Kinshasa Kin la belle |
|||
| |||
Mahali pa mji wa Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
|||
Majiranukta: 4°19′30″S 15°19′20″E / 4.32500°S 15.32222°E | |||
Nchi | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | ||
---|---|---|---|
Mkoa | Kinshasa | ||
Serikali | |||
- Governor | Gentiny Ngobila | ||
Eneo[1] | |||
- Jumla | 9,965 km² | ||
Mwinuko | 240 m (786.9 ft) | ||
Idadi ya wakazi (2009) | |||
- Wakazi kwa ujumla | 10,076,099 | ||
Tovuti: http://www.kinshasa.cd |
Kinshasa (jina la awali kwa Kifaransa: Léopoldville, na kwa Kiholanzi: Leopoldstad) ni mji mkuu na mji mkubwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, iliyojulikana kama Zaire miaka 1971-1997. Mji uko kwenye Mto Kongo[1] Ilihifadhiwa 28 Julai 2017 kwenye Wayback Machine..
Zamani pahali pa vijiji vya uvuvi, Kinshasa sasa ni jiji lenye idadi ya wakazi 10,076,099 mwaka 2009. Mji wa Brazzaville (wenye wakazi milioni 1.5 mwaka 2007 pamoja na makazi yake), [2] mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, hupatikana upande wa pili wa mto Kongo. Hivyo mrundiko wa Kinshasa-Brazzaville una wakazi karibu milioni 12.
Kwa sababu mipaka ya kiutawala huzunguka eneo kubwa, zaidi ya 60% ya ardhi ya mji iko katika asili ya mashambani, na eneo la mji hutwaa sehemu ndogo magharibi mwa jimbo. [3] [4]
Kinshasa imesawazishwa na Johannesburg kwa kuwa mji mkubwa wa pili katika Afrika kusini kwa Sahara na wa tatu kwa ukubwa katika bara zima baada ya Lagos na Cairo.
Mara nyingi huchukuliwa kuwa mji wa pili mkubwa zaidi duniani kwa idadi ya wazungumzaji wa Kifaransa baada ya Paris. Kama idadi ya watu itaendelea kukua kama sasa, Kinshasa itakuwa na wakazi wengi kuliko Paris kabla ya mwaka 2020. [5] [6]
Wakazi wa Kinshasa wanajulikana kama Kinois (Kifaransa) au Kinshasans (Kiingereza).
<ref>
tag; no text was provided for refs named Ville