Kinyemba

Kinyemba ni lugha ya Kibantu nchini Angola inayozungumzwa na Wanyemba. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kinyemba nchini Angola imehesabiwa kuwa watu 222,000. Pia kuna wasemaji wa Kinyemba nchi za Namibia na Zambia. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinyemba iko katika kundi la K20.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne