Kiokiek (pia Kiogiek) ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Kenya inayozungumzwa na Waokiek. Mwaka wa 2009 idadi ya wasemaji wa Kiokiek nchini Kenya imehesabiwa kuwa watu 79,000. Inasemekana kuna wasemaji wengine nchini Tanzania. Kwa vyovyote makundi mbalimbali ya Waokiek hawazungumzi lugha moja na wengine, na wengi wamebadili lugha kutumia lugha ya majirani zao kila mahali iwe Kimaasai, Kikuyu au Kiswahili. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiokiek iko katika kundi la Kinilotiki.