Kiokolod

Kiokolod ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia na Malaysia inayozungumzwa na Waokolod kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiokolod nchini Indonesia imehesabiwa kuwa watu 3390 na nchini Malaysia watu 1580. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiokolod iko katika kundi la Kiborneo-Kaskazini.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne