Kiorang-Kanaq

Kiorang-Kanaq ni lugha ya Kiaustronesia nchini Malaysia inayozungumzwa na Waorang-Kanaq. Mwaka wa 2008 idadi ya wasemaji wa Kiorang-Kanaq imehesabiwa kuwa watu 160 tu; maana yake lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiorang-Kanaq iko katika kundi la Kimalayiki. Wengine huiangalia kama lahaja ya Kimalay tu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne