Kipakanha kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wapakanha katika jimbo la Queensland. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea Kipakanha, yaani lugha imetoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipakanha kiko katika kundi la Kipaman.