Kipanytyima (pia Kibanyjima) ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wapanytyima katika jimbo la Australia Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kipanytyima 98 tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipanytyima kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.