Kiperai

Kiperai (pia Kitutunohan) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Waperai kwenye kisiwa cha Wetar. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiperai imehesabiwa kuwa watu 280 tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiperai iko katika kundi la Kitimor-Babar.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne