Kipintupi-Luritja

Kipintupi-Luritja ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wapintupi na Waluritja katika majimbo ya Northern Territory na Australia Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kipintupi-Luritja 1690. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipintupi-Luritja kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne