Kipokoot

Kipokoot ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Kenya na Uganda inayozungumzwa na Wapokoot. Mwaka wa 1994 idadi ya wasemaji wa Kipokoot nchini Kenya imehesabiwa kuwa watu 264,000. Pia kuna wasemaji 70,400 nchini Uganda kufuatana na sensa ya 2002. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipokoot iko katika kundi la Kinilotiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne