Lugha ya Kipoland | ||||||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kinazungumzwa katika: | Poland (38.5 milioni); Pia kuna wanzungumzaji katika Australia, Kanada, Uingereza, Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Belarus, Lithuania, Ukraine, Argentina, Brazil, Israel, na nchi nyingine kibao. | |||||||||||||||||||||||||
Waongeaji: | zaidi ya milioni 50 | |||||||||||||||||||||||||
Kama lugha rasmi: | ||||||||||||||||||||||||||
Nchi: | Poland | |||||||||||||||||||||||||
Uianishaji wa kiisimu: | ||||||||||||||||||||||||||
|
Kipoland (język polski, polszczyzna) ni lugha rasmi kwa nchi ya Poland. Kinafahamika zaidi kwa kuzungumzwa na watu waishio Maghari mwa Slovoni na ni lugha ya pili kwa ukubwa katika orodha ya Lugha za Kislavoni baada ya Kirusi. Ni moja kati ya lugha ngumu kujifunza kutokana na ugumu wa sarufi zake.
Katika historia, Kipoland kilikuwa lugha muhimu katika Ulaya ya Kati na Mashariki. Leo hii, kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 38.5 ikiwa kama lugha rasmi katika Poland. Pia kinazungumzwa kama lugha ya pili katika sehemu za magharibi mwa nchi ya Belarus, Lithuania, na Ukraine.
Kutokana na kuhamahama kwa watu wa Poland wa majira tofauti, mamilion ya waongeaji wa Kipoland wanaweza kupatikana katika nchi nyingi tu kama vile Australia, Kanada, Uingereza, Marekani, na sehemu nyingine nyingi tu. Kuna zaidi ya milioni 50 ya waongeaji wa Kipoland duniani.