Kireel (pia Kiatwot) ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Sudan Kusini inayozungumzwa na Wareel. Mwaka wa 1998 idadi ya wasemaji wa Kireel imehesabiwa kuwa watu 50,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kireel iko katika kundi la Kinilotiki.