Kiroka

Kiroka ni kata ya Wilaya ya Morogoro Vijijini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67204.


Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 14,307 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 21,853 [2] walioishi humo.

Kati yao walio wengi ni Waluguru wanaofuata dini ya Uislamu, lakini walau asilimia 10 ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (parokia ya Mtakatifu Kizito ya Jimbo Katoliki la Morogoro).

Kazi kubwa ya wananchi ni kilimo, hasa cha matunda mbalimbali.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Morogoro - Morogoro DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2015-03-21.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne