Kiroon ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Waroon kwenye kisiwa cha Roon. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kiroon imehesabiwa kuwa watu 1100. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiroon iko katika kundi la Kiyapen.