Kisegeju

Kisegeju ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wasegeju. Idadi ya Wasegeju imehesabiwa kuwa watu 15,000 lakini ni watu 7000 tu ambao bado wanajua kuongea Kisegeju, Wasegeju wengi wakitumia lugha za Kiswahili na Kidigo badala ya lugha yao. Kwa hiyo lugha imeanza kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kisegeju iko katika kundi la E70. Wengine wanasema kuwa ni sawa na Kidhaiso.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne