Kisheni ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Washeni. Mwaka wa 2004 idadi ya wasemaji wa Kisheni imehesabiwa kuwa watu sita tu, maana yake lugha imekaribia kutoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisheni iko katika kundi la Kikainji. Wengine husema kuwa lugha ya Kisheni ni sawasawa na lugha ya Kiziriya.