2°01′45″S 33°00′35″E / 2.029300°S 33.009796°E
Kisiwa cha Ukerewe ndicho kisiwa kikuu cha Tanzania ambacho kinapatikana katika Ziwa Viktoria, kiasi kwamba hilo linaitwa pia "Ziwa Ukerewe". Wenyeji wanakiita "Bukerebe".
Kikiwa na eneo la Km² 530 hivi, ndicho pia kisiwa kikuu cha Afrika kisicho cha baharini na kisiwa cha ziwani cha pili duniani kwa ukubwa.
Pamoja na visiwa vya jirani kinaunda Wilaya ya Ukerewe katika Mkoa wa Mwanza.
Wakazi wake ni 345,147.