Kismayu | |
Mahali pa mji wa Kismayu katika Somalia |
|
Majiranukta: 0°21′37″N 42°32′56″E / 0.36028°N 42.54889°E | |
Nchi | Somalia |
---|---|
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 183,300 |
Kismayu (pia: Kismayo au kwa Kisomali: Kismaayo) ni mji katika mkoa wa Jubbada Hoose wa Somalia mwambaoni mwa Bahari Hindi. Uko karibu na mdomo wa mto Juba. Kismayu ndio mji mkubwa katika eneo la Jubbaland. Mji wenyewe uko km 528 kusini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.
Katika mwaka wa 2011, Kismayu ilikadiriwa kuwa na wakaazi 183,300[1].