Kisori-Harengan

Kisori-Harengan ni lugha ya Kiaustronesia nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Wasori na Waharengan kwenye visiwa vya Sori na Harengan. Mwaka wa 1977 idadi ya wasemaji wa Kisori-Harengan imehesabiwa kuwa watu 570. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisori-Harengan iko katika kundi la Kioseaniki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne