Kitambotalo

Kitambotalo ni lugha ya Kiaustronesia nchini Vanuatu inayozungumzwa na Watambotalo kwenye kisiwa cha Santo. Mwaka wa 1981 idadi ya wasemaji wa Kitambotalo imehesabiwa kuwa watu 50 tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kitambotalo iko katika kundi la Kioseaniki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne