Kitanna-Kaskazini

Kitanna-Kaskazini ni lugha ya Kiaustronesia nchini Vanuatu inayozungumzwa na Watanna kwenye kisiwa cha Tanna. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kitanna-Kaskazini imehesabiwa kuwa watu 5000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kitanna-Kaskazini iko katika kundi la Kioseaniki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne