Kiteke-Ibali ni lugha ya Kibantu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumzwa na Wateke-Ibali. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kiteke-Ibali katika Jamhuri imehesabiwa kuwa watu 167,000. Pia kuna wasemaji 36,200 nchini Jamhuri ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiteke-Ibali iko katika kundi la B70.