Kitibeti ni lugha ya Kisino-Tibeti nchini Uchina, Uhindi na Nepal inayozungumzwa na Watibeti. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kitibeti nchini Uchina imehesabiwa kuwa watu 1,070,000. Pia kuna wasemaji 85,300 nchini Uhindi (2001) na wasemaji 4450 nchini Nepal (2011). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kitibeti iko katika kundi la Kibodish.