Kitswa

Kitswa ni lugha ya Kibantu hasa nchini Msumbiji inayozungumzwa na Watswa. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kitswa nchini Msumbiji imehesabiwa kuwa watu 1,160,000. Pia kuna wasemaji 20,000 nchini Afrika Kusini. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kitswa iko katika kundi la S50.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne