Kivunjajungu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kivunjajungu kijani wa Ulaya (Mantis religiosa)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Familia 16:
|
Vivunjajungu, vunjajungu au katamasikio ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa oda Mantodea (mantis = nabii, eidos = umbo) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wanatokea kanda za tropiki na nusutropiki na kusini (au kaskazini) kwa kanda za wastani. Kiwiliwili chao ni kirefu na chembamba. Miguu ya mbele imetoholewa kwa kukamata arithropodi wengine na hata vertebrata wadogo. Kwa kawaida koksa (coxa) za miguu ya wadudu ni fupi, lakini zile za miguu ya mbele ya vivunjajungu zimerefuka. Femuri na tibia zina miiba na meno inayowezesha mdudu kushika vizuri mawindo yake. Kama takriban wadudu wote vivunjajungu wana toraksi yenye sehemu tatu, lakini ile ya mbele, protoraksi, ni ndefu kuliko mbili nyingine pamoja na imeungwa vinamo na mesotoraksi. Hii inawezesha mdudu asogeze kichwa na miguu ya mbele pande zote wakati kiwiliwili kinatulia. Hata shingo ni kinamo na spishi kadhaa zinaweza kuzungusha kichwa kwa nyuzi 180.