Kiwajarri

Kiwajarri ni lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia inayozungumzwa na Wawajarri katika jimbo la Australia Magharibi. Katika sensa ya mwaka 2006, kulikuwa na wasemaji wa Kiwajarri 89 tu, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwajarri kiko katika kundi la Kipama-Nyungan cha Kusini-Magharibi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne