Kiwantoat ni lugha ya Kivuka-Guinea Mpya nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Wawantoat. Mwaka wa 1978 idadi ya wasemaji wa Kiwantoat imehesabiwa kuwa watu 8200, lakini tangu pale lugha imekaribia kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwantoat iko katika kundi la Kifinisterre.