Kiwardaman ni lugha ya Kigunwinyguan nchini Australia inayozungumzwa na Wawardaman katika jimbo la Northern Territory. Katika sensa ya mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kiwardaman ilihesabiwa kuwa watu 84 tu. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiwardaman kiko katika kundi la Kiyangmaniki.