Kiwarembori ni lugha ya Kipapua nchini Indonesia inayozungumzwa na Wawarembori. Mwaka wa 1989 idadi ya wasemaji wa Kiwarembori imehesabiwa kuwa watu 600, na wengi wameanza kuacha lugha yao, yaani Kiwarembori iko hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kiwarembori iko katika kundi la Kimamberamo ya Chini.