Kiyemba

Kiyemba ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Kamerun inayozungumzwa na Wayemba. Idadi ya wasemaji wa Kiyemba imehesabiwa kuwa watu 300,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyemba iko katika kundi la Grassfields ambalo linafanana na lugha za Kibantu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne