Kizazi cha dhahabu cha hip hop ni jina la kutaja enzi ya dhahabu katika anga la muziki wa hip hop ulioundwa katikati au mwishoni mwa miaka ya 1980—hadi mwanzoni au katikati mwa miaka ya 1990.[1] [2][3][4]Wanaotajwa kuwa miongoni mwa kizazi hiki walitokea mjini New York. Wakaipa jina la new-school, huku ikichukua sura mpya kabisa kuanzia ubora, ubunifu, na ushawishi wake katika hip hop kwa ujumla baada ya aina hiyo kujitokeza na kuimarika katika enzi ya old-school. Pia, inahusiana na maendeleo na mafanikio ya hip hop kama tasnia kuu ya muziki.
Mada zilikuwa za aina mbalimbali, huku muziki ukijaribu mitindo mipya na kutumia sampuli kutoka kwa rekodi za zamani ili kuleta mtazamo mpana na tofauti.
Wasanii wanaohesabiwa kuwa hasa ni wa kizazi hiki ni pamoja LL Cool J, Slick Rick, Ultramagnetic MC's,Jungle Brothers, Run-DMC, Public Enemy, Beastie Boys, KRS-One, DJ Jazzy Jeff & the Fresh Prince, Eric B. & Rakim, De La Soul, Big Daddy Kane, EPMD, Biz Markie, Salt-N-Pepa, Queen Latifah, Gang Starr, na A Tribe Called Quest.
Albamu na nyimbo za wasanii hawa ziliibuka sambamba na zile za wasanii wa awali wa gangsta rap kama Schoolly D, Ice-T, Geto Boys, na N.W.A, pamoja na muziki wa kimahaba wa 2 Live Crew na Too Short, pamoja na muziki wa amsha-amsha kutoka kwa wasanii kama Fat Boys, MC Hammer, na Vanilla Ice.[5][6][7]