Kizhuang-Zuojiang

Kizhuang-Zuojiang ni lugha ya Kitai-Kadai nchini Uchina na Vietnam inayozungumzwa na Wazhuang. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kizhuang-Zuojiang imehesabiwa kuwa watu milioni 1.5 nchini Uchina na watu 340,000 nchini Vietnam. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kizhuang-Zuojiang iko katika kundi la Kitai ya Kati.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne