Kiziriya

Kiziriya ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Waziriya. Idadi ya Waziriya imehesabiwa kuwa watu 2000 lakini wameacha lugha yao. Kwa hiyo, inawezekana kwamba lugha ya Kiziriya imeshatoweka kabisa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiziriya iko katika kundi la Kikainji. Wengine husema kuwa Kizirya ni sawa na lugha ya Kisheni.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne