Klaudi wa Condat | |
![]() Mt. Klaudi katika dirisha la kioo cha rangi | |
Nchi | Ufaransa |
---|---|
Kazi yake | Mtakatifu |
Klaudi wa Condat (au wa Besancon; Bracon, Jura, karibu Salins-les-Bains, Ufaransa, 607 hivi - 6 Juni 696 au 699) alikuwa padri, halafu mmonaki aliyepata kuwa abati wa Condat na hatimaye askofu wa Besancon, maarufu kwa miujiza[1][2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Juni[3].