Kobe | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kobe-chui (Stigmochelys pardalis)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusuoda 2:
|
Makobe ni wanyama wadogo hadi wakubwa wa oda Testudines katika ngeli Reptilia. Spishi zinazoishi baharini huitwa kasa.
Kiwiliwili chao kimefunikwa kwa gamba gumu liitwalo galili. Kwa kawaida galili hii ni yabisi, lakini kuna spishi zilizo na galili nyumbufu, zote spishi za maji. Kichwa, miguu na mkia inachomoza kutoka galili lakini katika spishi nyingi inaweza kuvutwa ndani, spishi za nchi kavu hasa.