Kodata (Chordata) | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ugwe wa neva wa samaki huyu (Pristella tetra) uonekana kupitia ngozi
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusufaila:':
|
Kodata (kutoka lugha ya kisayansi: Chordata) ni kundi kubwa la wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni.
Ugwe unaunganisha neva ambazo ni muhimu kwa mwili kwa jumla na neva za kila sehemu au kiungo zinatoka hapa. Ugwe wa neva unaenda sambamba na mhimili wa seli ambazo ni imara zaidi ama gegedu au mfupa.
Mhimili huu ni chanzo cha uti wa mgongo kwa wanyama wengi wa kundi hili na kiunzi cha mifupa cha ndani ya mwili.
Kodata waliendelea kutoka kwa wanyama wengine kama Arthropoda wenye kiunzi cha nje.
Katika uainishaji wa kisayansi Kodata ni faila ya wanyama (Animalia). Nusufaila yenye spishi nyingi ni Vertebrata. Hapa mhimili wa kati unaendelea kuwa uti wa mgongo.
Samaki, amfibia, reptilia na mamalia ni oda ndani ya vertebrata.