Kolumbani

Sura yake inavyoonekana katika dirisha la kioo cha rangi la kanisa la abasia ya Bobbio, Italia, ambapo alifariki akazikwa.

Kolumbani abati (kwa Kieire: Columbán, maana yake "Njiwa mweupe"; 540 - 23 Novemba 615) alikuwa mmonaki padri kutoka Ireland ambaye kwa upendo wa Kristo alijifanya mmisionari katika Ufaransa wa leo akieneza Ukristo wa Kiselti ukiwa pamoja na malipizi, na maungamo ya binafsi kwa padri.

Ni maarufu kwa kuanzisha monasteri ya Luxeuil, aliyoiongoza mwenyewe kwa kushika kikamilifu kanuni yake kali ya kitawa hadi alipolazimishwa kuhama, pamoja na nyingine nyingi katika nchi mbalimbali za Ulaya bara, ikiwemo ile ya Bobbio (Italia Kaskazini), iliyokuja kujulikana kwa nidhamu na elimu, ambapo ndipo alipofariki [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, hasa siku ya kifo chake, tarehe 23 Novemba[2].

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/30200
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne