Kongoni | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Kongoni
(Alcelaphus buselaphus cokii) | ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nususpishi 8:
| ||||||||||||||||||
![]() Misambao ya nususpishi za kongoni
|
Kongoni ni wanyamapori wakubwa wa jenasi Alcelaphus katika familia Bovidae. Kwa asili jina hili lilitumika kwa nususpishi A. buselaphus cokii lakini siku hizi nususpishi zote huitwa kongoni. Wanatokea savana za Afrika tu. Rangi yao ni ya mchanga lakini tumbo na matako ni nyeupe. Wana kichwa kirefu na pembe zao zimepindika na zina umbo wa zeze zikionwa kutoka mbele. Wanyama hawa hula manyasi.