Korogwe | |
Mahali pa mji wa katika Tanzania |
|
Majiranukta: 5°5′24″S 38°32′24″E / 5.09000°S 38.54000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Tanga |
Wilaya | Korogwe |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 86,551 |
Korogwe ni mji upande wa Kaskazini-Mashariki wa Tanzania ambao ni makao makuu ya Wilaya ya Korogwe. Tangu kupata halmashauri yake ni moja kati ya wilaya 11 za Mkoa wa Tanga kwenye pwani ya Tanzania.
Mwaka 2012 mji ulikuwa na wakazi 68,308 walioishi katika kata 8 za eneo lake.
Mwaka 2012 eneo la mji wa Korogwe lilitengwa na Wilaya ya Korogwe ya awali na kuwa na halmashauri yake ya pekee.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 86,551 [1].
Pia ni makao makuu ya Dayosisi ya Kanisa la Anglikana ya Tanga.