Kostabile, O.S.B. (Castellabate, Salerno, 1070 hivi - Cava de' Tirreni, Salerno, 17 Februari 1124) alijiunga na monasteri maarufu tangu utotoni akawa abati wake kuanzia mwaka 1122 hadi kifo chake.
Aliishi na kuongoza kwa upole na upendo wa ajabu hata akaitwa "blanketi" la ndugu.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Leo XIII tarehe 21 Desemba 1893.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 17 Februari[1].