Kyoto ni mji wa Japani uliokuwa mji mkuu wa nchi kati ya 794 na 1868. Ilikuwa makao makuu ya Tenno (Kaisari) wa taifa. Iko takriban kilomita 400 kusini magharibi ya Tokyo kwenye kisiwa cha Honshu.
Sasa Kyoto ni mji mkubwa wa tatu nchini iliwa na wakazi milioni moja na nusu. Ni makao makuu ya mkoa wa Kyoto. Kuna taasisi za utamaduni na elimu pamoja vyuo vikuu.
Kyoto ni kati ya miji ya kale ya Japani. Kuna majengo mengi ya kihistoria kama mahekalu, majumba ya matenno na nyumba za kidesturi. Majengo kadhaa yameigizwa na UNESCO katika orodha ya urithi wa dunia.
Mazingira ya Kyoto pana milima mingi. Imepoteza cheo cha mji mkuu wakati Tenno Meiji alipohamisha makao yake kutoka hapa kwenda boma la Edo iliyokuwa Tokya baadaye.