Lahaja

Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainishwa na jamii au jiografia.

Lahaja za lugha moja zinakaribiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati.

Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi (upekee wa uzungumzaji), si lahaja.

Uchambuzi na uchanganuzi wa lahaja ni tawi la isimujamii.

Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo:

  1. vipengele vya sera (lahaja rasmi na lahaja sanifu)
  2. vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika
  3. vipengele vya kijamii (lahaja jamii na lahaja tabaka)
  4. vipengele vya eneo

Mfano wa lugha yenye lahaja mbalimbali ni Kiingereza na lahaja zake zinavyozungumzwa tofauti Uingereza, Marekani, Uhindi, Australia na maeneo mengine.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne