Lahaja sanifu (au lugha sanifu) ni lahaja ambayo imeteuliwa kutoka lahaja nyingine kutumika kwa upana zaidi kuliko lahaja za kawaida. Lahaja sanifu hutumika hasa kwa mawasiliano baina ya wasemaji wa lahaja tofauti za lugha moja; tena, hutumika katika shughuli zilizo rasmi. Ili kuwa sanifu, lahaja teule hufanyiwa marekebisho madogomadogo upande wa matamshi, sarufi na semantiki. Marekebisho hayo yanawezekana kutokea bila watu kujua.