Lakshadweep ni eneo la muungano la jamhuri ya India. Linaundwa na funguvisiwa la bahari ya Hindi lililojulikana kwanza kama Laccadive. Liko kilometa 200/440 kutoka pwani ya kusini-magharibi ya India.
Eneo lote ni la kilometa mraba 32 tu.
Makao makuu ni Kavaratti.
Wakazi ni 65,473 (2011). Wengi wao wana asili ya Kerala, na dini kubwa ni Uislamu.