Lecrae | |
---|---|
![]() Lecrae na Akon, mnamo 2013
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Lecrae Moore |
Aina ya muziki | Kikristo, Nyimbo za Kikristo |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Studio | Reach Records |
Tovuti | http://www.reachrecords.com/ |
Lecrae Moore (amezaliwa 9 Oktoba, 1979) ni msanii wa Kikristo[1] mwenye mkataba na Reach Records.[2]
Lecrae anaishi mjini Atlanta, Georgia akiandaa matukio mbalimbali ya muziki, akijitolea kufanya kazi katika jela ya vijana, kujishirikisha katika shirika la Kids Across America Kamps huko Branson, Missouri na akijishughulisha na Reachlife Ministries.[3] Pia, yeye ni mwanachama wa 116 Clique, Lecrae anahubiri Injili katika vyuo vikuu mbalimbali na kumbi mbalimbali za jamii.
Lecrae amepokea uchaguzi wa kuwa mshindani kwa tuzo mbili katika tuzo za kila mwaka za GMA Dove. Alipata uchaguzi kwa wimbo wake Jesus Muzik,aliomshirikisha Trip Lee na kwa albamu yake After the Music Stops[4]. Yeye ,hivi majuzi,alikuwa amechaguliwa kama mshindani kwa tuzo ya Albamu ya Sanaa ya Rap ya Mwaka katika tuzo za arubaini za GMA Dove. Magazeti mbalimbali,likiwemo Rapzilla[5] yameaona na kusifu mtindo wake tofauti na albamu yake ya pili After the Music Stops iliitwa "mojwapo ya albamu bora sana ya 2006[6]". Nyimbo zake zinaonyesha werevu wake lakini zinahakikisha ujumbe umewasilishwa.
Katika muziki wake, Lecrae anatumia neno "Crunk" kwa kumaanisha hisia nzuri anayohisi Mkristo.[7] 8 Oktoba 2008, albamu ya tatu ya Lecrae, Rebel, iliingia chati ya Billboard ikwa # 60,huku ikiwa imenunuliwa na watu 9,800. Rebel ikawa # 3 katika iTunes na kushikilia nafasi ya kwanza katika chati ya Kikristo ya Billboard kwa wiki mbili,albamu ya rap ya kwanza kufanya hivyo. Lecrae ana video nne vya nyimbo zake:Jesus Muzik, Praying For You, Don't Waste Your Life, ambayo ilishinda Video ya Mwaka katika tuzo za GMC na hapo Oktoba 2009 alitoa video ya wimbo wake Go Hard.