Leo wa Catania

Picha takatifu inayomchora Mt. Leo.

Leo wa Catania (Ravenna, Emilia-Romagna, 709 hivi - Catania, Sicilia, 20 Februari 789) alikuwa askofu wa 15 wa Catania, leo nchini Italia, maarufu kwa huruma yake kwa maskini na kwa miujiza mingi.

Ujanani alijiunga na Wabenedikto, lakini alipohamia Italia Kusini alifanywa shemasi mkuu wa Reggio Calabria hadi alipochaguliwa kuwa askofu. Katika dhuluma ya serikali ya Bizanti dhidi ya walioheshimu picha takatifu alilazimika kuhamahama lakini hatimaye alirudi madarakani.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Februari[1][2][3].

  1. Martyrologium Romanum
  2. Great Synaxaristes: (Kigiriki) Ὁ Ἅγιος Λέων ὁ Θαυματουργός Ἐπίσκοπος Κατάνης. 20 Φεβρουαρίου. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ. Retrieved: 2013-06-24.
  3. St Leo the Bishop of Catania in Sicily. OCA - Lives of the Saints. Retrieved: 2013-06-24.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne